John 1:26-31

26 aYahya akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji,
Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji.
lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua.
27 cYeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”

28 dMambo haya yote yalitukia huko Bethania, ng’ambo ya Mto Yordani, mahali Yahya alipokuwa akibatiza.

Isa Mwana-Kondoo Wa Mungu

29 eSiku iliyofuata, Yahya alimwona Isa akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30 fHuyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ 31 gMimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”

Copyright information for SwhKC